Utangulizi
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeanza kuratibu maandalizi ya Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050. Serikali inatambua kuwa, maono na maratajio ya watanzania na mbinu za kuyafikia zinatokana na watanzania wenyewe kupitia ushirikishwaji madhubuti katika maandalizi na utekelezaji wa mipango ya maendeleo. Ili kuhakikisha Dira hiyo inabeba maono na matarajio ya watanzania kwa miaka 25 ijayo, ni muhimu wananchi na wadau wote wa maendeleo kushirikishwa kikamilifu katika mchakato wa maandalizi ya Dira tangu hatua za awali hadi kukamilika kwake.
Kwa kuzingatia umuhimu huo, unaombwa kutoa maoni yako kwa kuzingatia vipengele vya dodoso hili. Aidha, unaombwa kuongeza maelezo na taarifa za ziada ambayo ni muhimu kuzingatiwa katika Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050. Taarifa utakazotoa zitatumika katika maandalizi ya Dira na hivyo unahakikishiwa usiri wa taarifa utakazozitoa. Tunashukuru kwa ushirikiano wako.